Ripoti mpya ya Human Rights Watch
pamoja na tume ya kupigania haki za kibinadamu KNHRC inataka maafisa
waliokiyuka haki za kibinadamu wakati wa misako baada ya mashambulizi ya
kigaidi wachunguzwe.
Mshauri wa tume ya
KNHRC Lilian Kantai amesema kumekuwa na madai ya maafisa wa usalama kushiriki mauaji ya washukiwa wa ugaidi kinyume na
sheria.
Bi. Kantai amesema
washukiwa walizuiwa katika mazingira duni huku wakipigwa.
Bi. Kantai ameongeza
kulikuwa na madai ya watu kutoka jamii ya Wasomali kulengwa wakati wa misako.
Kulingana na utafiti
huo vitengo vya usalama vimeripotiwa kuchukua muda mrefu kufika katika maeneo
ya dharura.
No comments:
Post a Comment