Monday 15 June 2015

RIPOTI YA HAKI ZA BINADAMU



Ripoti mpya ya Human Rights Watch pamoja na tume ya kupigania haki za kibinadamu KNHRC inataka maafisa waliokiyuka haki za kibinadamu wakati wa misako baada ya mashambulizi ya kigaidi wachunguzwe.

Mshauri wa tume ya KNHRC Lilian Kantai amesema kumekuwa na madai ya maafisa wa usalama kushiriki  mauaji ya washukiwa wa ugaidi kinyume na sheria.

Bi. Kantai amesema washukiwa walizuiwa katika mazingira duni huku wakipigwa.

Bi. Kantai ameongeza kulikuwa na madai ya watu kutoka jamii ya Wasomali kulengwa wakati wa misako.

Kulingana na utafiti huo vitengo vya usalama vimeripotiwa kuchukua muda mrefu kufika katika maeneo ya dharura.

No comments:

Post a Comment